Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, naomba niwapongeze Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Watendaji na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mawasiliano, katika Jiji la Dodoma eneo la pembezoni Kata ya Mbalawala, Kijiji cha Lugala – Matangizi hakuna mawasiliano ya simu hali ambayo inasababisha wagonjwa kutopata huduma kwa haraka kutokana na umbali wa eneo hilo. Naomba wananchi hawa wapatiwe mawasiliano ya simu ili waondokane na changamoto hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Seminari, mnamo mwaka 2015 wakati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mgombea wa Urais aliwaahidi wananchi wa Jimbo la Segerea kuwa barabara ya Segerea - Seminari - Majumbasita (km 3) itajengwa kwa kiwango cha lami. Hata hivyo, barabara hiyo haina hata dalili ya kutengenezwa kwa kiwango cha lami. Naomba Serikali itekeleze ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nirudie kuwashukuru sana watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya.