United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Watumishi wa Bunge wamewasili Mkoa wa Lindi tarehe 31 Julai na kupokelewa na ofisi ya RAS Mkoani humo, kwaajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu Masuala ya Bunge kwa shule za Msingi na Sekondari.
Watumishi hao walianza kwa kutoa elimu kwa Sekondari ya Lindi na kesho yake tarehe 01 Agosti walielimisha shule nne, Wailes na Mtuleni shule za Msingi kwa upande wa sekondari WAMA Sharif na Angaza.
Watumishi hao wanatarajia kuwepo Mkoa wa Lindi hadi tarehe 11 Agosti 2023.