United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club
wamewasili Jijini Juba nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kushiriki katika mashidano
ya michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kuanza
tarehe 25 Novemba hadi 2 Disemba 2022.
Awali
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu aliwakabidhi Wachezaji hao
bendera ya Taifa na Bunge kwa niaba ya
Spika wa Bunge. Tukio hilo lilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar
es Salaam.
Aidha
akizungumza na Wachezaji hao kabla ya kuwakabidhi bendera Naibu Spika aliwaasa
kudumisha heshima ya taifa pamoja na nidhamu wakati wote wa mashidano.
"Nendeni
mkadumishe heshima ya taifa letu na
mkalitangaze, kama taifa tuna fursa mbalimbali zikiwemo za utalii,"
alisema Naibu Spika.
Pia
Naibu Spika aliwaambia wachezaji hao kwamba wanatarajiwa kurudi na vikombe
katika michezo mbalimbali ambayo watashiriki.