United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Kufuatia uwepo
wa Ugonjwa wa Corona hapa nchini, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikitoa elimu na miongozo mbalimbali ya
kujikinga na maambukizi pamoja na hatua za kuchukua ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi
ya ugonjwa huo. Miongoni mwa hatua
inayosisitizwa ni kuepusha mikusanyiko ya watu.
Kamati 14
za Kudumu za Bunge zinakutana tarehe 16 – 29 Agosti, 2021. Vikao hivi vya
Kamati vinahusisha mkusanyiko wa Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Bunge,
Watendaji wa Serikali, Waandishi wa Habari na Wageni wengine mbalimbali.
Katika
kutekeleza kwa vitendo tahadhari za kiafya zinazotolewa na Serikali, Uongozi wa
Bunge umeweka utaratibu wa uendeshaji wa Vikao vya Kamati kama ifuatavyo:-
a. Kumbi 7 kubwa ndizo zitatumika kwa Vikao vya Kamati;
b. Kamati zitakutana kwa kupishana yaani, saa 3:00 Asubuhi – 7:30 Mchana,
Kamati 7 na saa 8:00 Mchana hadi saa
12:30 Jioni, Kamati 7 zilizosalia;
c. Kila Kamati itafanya vikao kwa namna inayozingatia muda uliopangwa ili
kutoathiri muda wa kuanza kwa vikao vya Kamati nyingine; na
d. Idadi ya Watendaji wanaokuja na Waziri kwenye vikao vya Kamati isizidi
Maafisa 5 wa Wizara kwa kikao.
Aidha, Wageni watakaoruhusiwa Bungeni kwa kipindi hiki ni Wageni wanaofika Ofisini kwa shughuli za kiofisi, Waandishi wa Habari waliosajiliwa kwa ajili ya kutoa habari za Kibunge pamoja na Wadau watakaohudhuria Vikao vya Kamati kwa ajili ya kutoa maoni ambao wataelekezwa na Kamati inayohusika kabla ya Kikao cha kupokea maoni.
Hon. Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Songea Mjini (CCM)