United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania

Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Waheshimiwa Wabunge ambao hawatachanja chanjo ya UVIKO-19 hawataruhusiwa kuingia Bungeni.
Tunapenda
kuujulisha umma kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani maelekezo
yaliyopo na ambayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb) amekuwa akisisitiza ni kuwahimiza Waheshimiwa
Wabunge kujitokeza kuchanja chanjo hiyo kwa hiari yao.
Aidha,
Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu utakaowawezesha Waheshimiwa Wabunge wote
kupata chanjo hiyo katika viwanja vya Bunge kwa hiari yao wenyewe.
Hivyo,
Waheshimiwa Wabunge wanasisitizwa kutumia hiari hiyo kujitokeza ili kupata
chanjo kwa ajili ya kujikinga wao wenyewe na kuwakinga wengine.