United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika
kutangaza kifo cha Mbunge wa Ushetu (CCM) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Mhe. Elias John Kwandikwa, kilichotokea tarehe 02 Agosti, 2021 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa
matibabu.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko
makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Elias John Kwandikwa (Mb). Natoa pole kwa Serikali, Waheshimiwa
Wabunge, familia na wananchi wa Jimbo la Ushetu. Mwenyezi Mungu awape Moyo wa
ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.” amesema Mhe. Spika.
Taarifa zaidi zitatolewa baada ya Ofisi kupata utaratibu na ratiba
ya mazishi kutoka Serikalini.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina