United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) amezindua Bunge Marathon itakayofanyika tarehe 13 Aprili 2024 Dodoma, leo tarehe 09 Novemba 2023 ukumbi wa Msekwa Dodoma
Akiwa anasoma hotuba yake, Mheshimiwa Spika alisema mbio hizi zitakuwa na lengo mahususi ya kuchangisha rasilimali fedha na mali kwa lengo maalum litakalokuwa linapangwa kila mwaka.
Pia alisema kwamba Bunge limekuwa linajihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kujenga shule ya wasichana ya Bunge ambayo inafanya vizuri katika taaluma ya elimu.
Aliongezea kwa kusema kwamba ili kufanikisha jambo hili, Ofisi ya Bunge inahitaji ushirkiano kutoka katika Taasisi na Makampuni mbalimbali binafsi na Serikali.
Alimalizia kwa kushukuru wadau mbalimbali waliofika kwenye Uzinduzi huo pamoja na Wabunge na viongozi waliokuwepo.