Parliament of Tanzania

Spika wa Bunge la Rwanda atembelea Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatile amewasili Dodoma kwa ziara ya siku tatu katika Bunge la Tanzania na baadhi ya maeneo ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Donatile aliwasili Juni 9, mwaka huu na kupokelewa na wenyeji wake Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, baadhi ya Viongozi na Maafisa wa Bunge.

Akizungumza kuhusu ugeni huo Spika Ndugai alisema kumekuwa na mahusiano mazuri kati ya Bunge la Rwanda na Bunge la Tanzania na mara kadhaa Kamati za Bunge la Tanzania zimekuwa zikienda Rwanda na kujifunza jinsi wanavyoendesha shughuli zao na sasa nao wamepata fursa ya kuja Tanzania kujifunza.

Spika wa Rwanda ambaye ameambatana na wabunge wawili na Maofisa watatu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge, Naibu Spika, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Wabunge wanawake na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's