United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
SPIKA wa Bunge,Mhe. Job Ndugai amesema Kamati ya Uongozi ya Bunge inalo jukumu kubwa la kujadili na kumshauri Spika kuhusu mambo yanayohusu Shughuli za Bunge.
Mhe. Ndugai ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati akifungua semina ya Wenyeviti wa Kamati za Bunge ya kuwajenge uwezo wabunge.
Amesema majukumu hayo ya kumshauri Spika yameainishwa katika nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Akizungumzia mafunzo hayo amesema yatasaidia kuboresha utendaji wa Kamati ya Uongozi na Bunge kwa ujumla.
"Katika siku za usoni pia tutaandaa mafunzo haya kwa vitendo nje ya nchi,lipo Bunge moja tu Tanzania na hivyo mafunzo pekee ya vitendo ni kwa kutembelea mabunge ya wenzetu,"amesema.
Amesema mafunzo hayo kwa Wenyeviti wa Kamati za Bunge yamejikita katika mchakato wa utungaj sheria na uchambuzi wa miswada na mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya Serikali na Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015.
"Maeneo mengine ni majukimu ya Wenyeviti wa Kamati za Bunge na namna ya kuzungumza mbele ya hadhara,namna ya kutumia vyombo vya Habari wakati wa shughuli za kamati na mabadiliko,maboresho na hatma ya Bunge,"amesema.
Mhe. Spika pia amelishukuru Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wao wa Kuwajengea Uwezo Wabunge (LSP) Kwa kutoa mafunzo kwa wabunge na watumishi ambayo yamekuwa na tija Kubwa.