United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Bunge la Tanzania linatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Mtandao wa Wabunge Wenye Mahitaji Maalum wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika (CPwD). Mkutano wa uzinduzi wa Mtandao huo ulifanyika Nairobi nchini Kenya, Mwezi Oktoba, 2021.
CPwD ni mojawapo ya Chombo cha Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Madola kilichoanzishwa mwaka 2017. Lengo kuu la Mtandao huu ni
kuwezesha shughuli na programu zinazolenga kuongeza uwakilishi wa watu wenye
ulemavu kwenye Mabunge na kuhakikisha kuwa masuala yanayohusu ulemavu
yanazingatiwa kwenye mipango na shughuli mbalimbali za Mabunge.
Ili kufikia lengo hilo, mnamo mwaka 2020, Mtandao huu ulianzisha Kamati
ya Utendaji inayoundwa na Mwakilishi mmoja kutoka Kanda zote tisa (9) za Mabunge
ya Jumuiya ya Madola. Kazi za Wawakilishi hawa ni kutetea haki za watu wenye
ulemavu kwenye Kanda husika na kuwakilisha maslahi yao ndani ya CPA.
Mkutano wa pili wa CPwD utafanyika tarehe 14 – 18 Novemba, 2022 katika Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson. Mkutano utahusisha Wabunge
wenye mahitaji maalum kutoka Mabunge ya nchi wanachama wa CPA Kanda ya Afrika.
Mabunge hayo ni Afrika ya Kusini, Botswana, Cameroon, Eswatini, Gambia,
Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra
Leone, Seychelles, Tanzania, Uganda, Zambia na Mauritius.
Aidha, kauli mbiu ya Mkutano huo ni ‘Parliamentarians and PwDS as
champions of inclusion and accessibility to Public and Private Sectors.’
Mada sita (6) zitakazojadiliwa ni zifuatazo:-
i.
A review of education system for PwDs: A case
study of Tanzania;
ii.
Towards increased PwDs representation in
Parliaments: Legal and Constitutional Amendments;
iii.
Promoting economic empowerment and entrepreneurship
to advance the participation of PwDs in the labour market;
iv.
The role of Parliaments in facilitating the Needs
of Persons with Disabilities;
v.
Empowering Persons with Disabilities through ICT:
Challenges and Opportunities; na
vi.
Sexual and
Reproductive Health Rights for women with disabilities.