United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi na Mbili umeanza tarehe 2 Februari 2021 Jijini Dodoma na unatarajiwa kufanyika hadi tarehe 12 Februari, 2021.
Aidha, kabla ya kipindi cha Maswali na Majibu, Spika wa Bunge, Mhe.
Job Ndugai aliwatambulisha Waheshimiwa Wabunge ambao waliapishwa kwa nyakati
tofauti nje ya Ukumbi wa Bunge.
Wabunge hao ni Wabunge watano walioteuliwa na Mhe.
Rais, Wabunge wanne kutoka ACT Wazalendo na Wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Pamoja na mambo mengine Shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huu ni
kama ifuatavyo:-
1. Maswali
Katika
Mkutano huu wastani wa maswali 125 ya kawaida na Maswali 16 ya papo kwa papo
kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge kwa mujibu wa
Kanuni ya 45 (1) na 44 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020.
2.
Hotuba ya Rais
Kwa mujibu wa Kanuni ya 36 (3) ya Kanuni za Bunge,
Toleo la Juni, 2020 Waheshimiwa Wabunge watapata fursa ya kujadili Hotuba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na
Mbili.
3.
Kamati ya Mipango
Katika Mkutano huu, Bunge litakaa kama Kamati ya
Mipango ili kujadili na kushauri kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Taifa
unaokusudiwa kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 113 (2) ya Kanuni za Bunge,
Toleo la Juni, 2020, Bunge hukaa kama Kamati ya Mipango katika katika Mkutano
wa Mwezi Oktoba – Novemba kila mwaka isipokuwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge
Jipya. Kwa kuwa Mkutano wa Novemba, 2020 ulikuwa wa Kwanza wa Bunge hili, hivyo
Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango katika Mkutano huu wa Pili.