Parliament of Tanzania

Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge la Kumi na Moja umeanza tarehe 3 Septemba na unatarajiwa kufanyika hadi tarehe 13 Septemba 2019, Jijini Dodoma.


Katika kikao cha Kwanza cha Mkutano huo mbali na Maswali ya kawaida shughuli zingine zilizofanyika ni pamoja na Kiapo cha Uaminifu cha Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu.


Pia, katika kikao cha kwanza lilosomwa na kupitishwa Azimio la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na Kuendesha Vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo.

Aidha katika Mkutano huu Miswada inayotarajiwa kusomwa na kujadiliwa ni pamoja na;-


· Muswada wa Sheria ya Serikali Mtandao wa Mwaka 2019 [The e-Government Bill, 2019]


· Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.4), Bill, 2019]


· Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5), Bill, 2019]


· Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.6) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.6), Bill, 2019]

Kwa upande mwingine katika Mkutano huu Bunge pia linatarajiwa kujadili na kuridhia Maazimio yafuatayo yaliyowasilishwa na Serikali kwa Mheshimiwa Spika.


· Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.


· Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Kigosi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi.


· Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Ugalla kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla.


· Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (The Protocol for Protection of New Varieties of Plant [Plant Breeder’s Rights] in the Southern African Development Community – SADC)


· Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezesha Upatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa Watu Wasioona, Wenye Uoni Hafifu au Ulemavu Unaofanya Mtu Kushindwa Kusoma wa Mwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Published Works for Persons who are Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled (MVT) 2013).


· Azimio la Kuridhia Mkataba wa Minamata Kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)


· Azimio la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisiasa katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety).


Kabla ya Bunge kuahirishwa pia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo itawasilisha kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's