United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Umoja wa Wabunge Vijana umemchagua Mheshimiwa Zainab Katimba (Mb) kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo katika uchaguzi uliofanyika Jijini Dodoma.
Viongozi wengine wa Umoja huo ambao wamechaguliwa katika
uchaguzi huo ni Mheshimiwa Salome Makamba (Mb) amechaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Ramadhan Ramadhan (Mb) amechaguliwa kuwa Katibu
na Mheshimiwa Dkt. Alfred Kimea (Mb) amechaguliwa kuwa Mwekahazina.
Aidha waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja huo ni Mheshimiwa Khadija Taya (Mb), Mheshimiwa Latifa Juwakali (Mb) na Mheshimiwa Maryam Omar Said (Mb).