Parliament of Tanzania

MHESHIMIWA SPIKA AWAAPISHA WABUNGE WANNE WA ACT WAZALENDO

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, amewaapisha Waheshimiwa Wabunge wanne kutoka Chama cha ACT Wazalendo katika Viwanja vya Bunge Jijiini Dodoma.

Waheshimiwa Wabunge walioapishwa ni Khatibu Said Haji, Salum Mohamed Shafi, Omar Ali Omar na Khalifa Mohamed Issa.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Mheshimiwa Spika aliwapongeza Wabunge hao kwa kukamilisha azma yao ya kuwakilisha wananchi huku akisisitiza kwamba majina ya Wabunge waliapishwa leo ameletewa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Aidha, Mheshimiwa Spika alisema kuapishwa kwa Wabunge hao ni mchakato wa kuendelea kukamilisha Bunge ambapo hadi sasa kati ya Wabunge 393 ni Wabunge kumi tu ambao bado mchakato wao haujakamilika.

“Kwa hiyo tunayo “Quorum” (akidi) ya kutosha kuweza kuendesha Bunge na kufanya maamuzi yoyote.

“Uongozi wa Bunge utalinda haki zenu, ni wajibu wa Spika kuwalinda Wabunge walio wachache kuhakikisha wanapata haki ya kusikilizwa halafu walio wengi waatamua, tutahakikisha haki inatendeka, Bunge liko imara kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania.

“Wabunge wapo majimboni wanaendelea kuchapa kazi na naendelea kusisitiza wote waliapishwa ni wabunge kamili wakati utakapofika wafike Bungeni kuendelea kutekeleza majukumu yao,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mheshimiwa Khatibu alimshukuru Mheshimiwa Spika kwa kukubali kuwaapisha na kwamba kuchelewa kwao kula kiapo cha uaminifu sio kwamba ilikuwa ni kukwepa majukumu bali ilikilazimu Chama chao kupitia maoni ya wanachama kujiridhisha kwa kila jambo wanalaomua kulifanya.

“Hivyo basi, uwepo wetu hapa una baraka za Mwenyezi Mungu, una baraka za Chama chetu na baraka za wapiga kura,” alisema.

Aidha, aliwapongeza Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hussen Ali Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais,Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema makubaliano hayo yataiweka Zanzibar katika hali ya amani na utulivu na kwamba maamuzi hayo yamezingatia maslahi mapana ya Taifa na Wazanzibar kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera,Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mheshimiwa Jenista Mhagama alimshukuru Mungu kwa kuendelea kuwadhihirishia Watanzania na Ulimwengu kwamba Nchi inajali umoja na mshikamano wa kitaifa.

Aliwapongeza Waheshimiwa Wabunge walioteuliwa na kuahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament