United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mbunge wa Kawe, Mheshimiwa Josephat Gwajima amehojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku shauri lake likitarajiwa kuendelea Jumatano tarehe 25 Agosti, 2021.
Akizungumza mara baada ya mahojiano hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Emmanuel Mwakasaka alisema Mheshimiwa Gwajima ametoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati ambayo kazi yake ni kuchunguza Mbunge anayekiuka maadili na Kanuni za Bunge.
Alisema Kamati ikimaliza kazi yake itapeleka mapendekezo yake kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa kuwa ndiye mwenye shauri hilo.
Alisema kitendo cha Mheshimiwa Gwajima kuhojiwa kwa siku mbili ni cha kawaida kwa kuwa walikutana na mbunge huyo mchana hivyo hawakuweza kumaliza.
Mheshimiwa Gwajima alihojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa muda wa takribani saa mbili.