United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi, ndc amewataka wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi kufanya kazi kwa ushirikiano na watu walio chini yao na hivyo kulifanya Bunge kuwa sehemu nzuri ya kufanya kazi kwa wale wanaowatumikia.
Katibu wa Bunge alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya
kuwajengea uwezo wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi wa Ofisi ya Bunge yanayotolewa
na Taasisi ya Uongozi, katika Ofisi Ndogo ya Bunge Zanzibar
“Sisi viongozi tunatakiwa kufanya Bunge kuwa sehemu nzuri ya
kufanyia kazi na tunaowatumikia wawe na furaha,” alisema.
Aidha, alimshukuru Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa
kuona umuhimu wa mafunzo hayo hivyo kuwaruhusu viongozi hao wote kushiriki mafunzo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,
Kadari Singo alimpongeza Bi. Nenelwa Mwihambi kwa kuwa mwanamke wa kwanza
kuteuliwa kushika nafasi ya Katibu wa Bunge.
Alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa viongozi hao kwa kuwa kwa
taasisi waliyopo wanaushawishi katika
namna moja au nyingine katika maendeleo ya Taifa.
Hon. Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika
Newala Mjini (CCM)