United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania

Kamati
za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Jijini Dodoma Jumatatu tarehe 8 Machi 2021 kwa
ajili ya vikao vinavyotangulia kabla ya Mkutano wa Tatu wa Bunge uliopangwa kuanza
tarehe 30 Machi, 2021.
Kwa
mujibu wa ratiba Kamati hizo zitakuwa na shughuli zifuatazo;
i)
Kupokea mapendekezo
ya Serikali kuhusu Mpango, kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2021/2022 kwa mujibu wa Kanuni ya 116(1) ya Kanuni za Kudumuza Bunge Toleo la
Juni, 2020. Wabunge wote watahusika na shughuli hii;
ii)
Kutembelea
na Kukagua Utekelezaji wa Miradi iliyotengewa
fedha kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ili kuzingatia masharti ya Kanuni ya 117(1)
ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020. Wajumbe wa Kamati za Kisekta watahusika
na shughuli hii;
iii)
Ziara za
Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Umma kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Serikali Kuu na Taasisi za Umma ili kuzingatia masharti ya sehemu ya Nne ya Nyongeza
ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020;
iv)
![]()
Uchambuzi wa taarifa za Uwekezaji uliofanywa na Serikali
kupitia mashirika, taasisi na Kampuni ambazo Serikalii na Hisa pamoja na ziara
ya kukagua shughuli za uwekezaji zilizofanywa na Serikali kupitia Mashirika,
Taasisi na Kampuni ambazo Serikali ina Hisa. Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji
ya Umma watahusika na shughuli hii;
v)
Uchambuzi
wa Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa
fedha 2021/2022 kwa mujibu wa Kanuni ya 117(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge
Toleo la Januari, 2020. Wajumbe wa Kamati za Kisekta, Kamati ya Bajeti na Kamati
ya Masuala ya Ukimwi watahusika na shughuli hii;
vi)
Uchambuzi
wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Pili wa Bunge ili kutekeleza
masharti ya kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge
Toleo la Juni, 2020;
vii)
Mashauriano
kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti kuhusu masuala muhimu yatakayokuwa
yamejitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa uchambuzi wa Taarifa za utekelezaji
wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2020/21. Shughuli hii ni kwa mujibu wa
Kanuni ya 117(5) na 117(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020.