Parliament of Tanzania

Kamati za kudumu za Bunge zaanza kukutana Jijini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana tarehe 13 Januari, 2020, Jijini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 28 Januari, 2020.

Shughuli zinazotarajiwa kutekelezwa na Kamati katika kipindi hiki ni pamoja na:-

a) Kupokea na Kujadili Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Majukumu na Bajeti ya Serikali kupitia Wizara na Taasisi zake. Shughuli hii itatekelezwa na Kamati za Kisekta na Bajeti.

b) Kushughulikia hoja mbalimbali za Ukaguzi kama zilivyoripotiwa katika Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa ya Mdhibit i na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha unaoishia Juni, 2018. Jukumu hili litatekelezwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

c) Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) itafanya ziara za ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika baadhi ya miradi ya maendeleo.

d) Kupokea taarifa kuhusu namna hisa za Serikali zinavyosimamiwa katika mashirika na Taasisi mbalimbali ambazo Serikali ina hisa pungufu ya asilimia hamsini. Shughuli hii itatekelezwa na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

e) Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Mezani wakati wa Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge. Shughuli hii itatekelezwa na Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo.

f) Kuandaa taarifa ya Kamati kuhusu shughuli zilizotekeleza katika kipindi cha kuanzia Januari, 2019 hadi Januari, 2020. Shughuli hii itatekelezwa na Kamati zote.

Ratiba za Shughuli za Kamati za Bunge pamoja na maeneo ambayo Kamati hizo zitafanya ziara zinapatikana katika Tovuti ya Bunge.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's