United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Vikao vya kawaida vya
Kamati za Kudumu za Bunge vimeanza kufanyika tarehe 7 Agosti, 2023 Jijini Dodoma
na vinatarajiwa kuhitimishwa tarehe hadi 25 Agosti, 2023. Vikao hivi
vinafanyika kwa ajili ya maandalizi ya
Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge utakaonza tarehe 29 Agosti, 2023.
Shughuli
za Kamati katika kipindi hicho ni pamoja na: -
i) Uchambuzi
wa Miswada miwili (2) ya Sheria utakaofanywa na Kamati mbili: Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Bajeti;
ii) Uchambuzi
wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge;
iii) Uchambuzi
wa Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni,
2022;
iv) Uchambuzi
wa Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa lengo la kuliwezesha Bunge
kufuatilia ufanisi na tija kwa Mitaji ya Serikali kwenye mashirika mbalimbali
na taasisi; na
v) Uchambuzi
wa Taarifa za Utendaji za Wizara kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza
jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali.