Parliament of Tanzania

KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATOA SIKU 90 WIZARA KUSHUGHULIKIA MADENI YOTE

Agizo hilo limetolewa Mkoani Mbeya leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na utalii Mhe. Dkt.Aloyce Kwezi
wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua Mradi Na.2326 wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika Mkoa wa Mbeya.

"Hapa Mbeya tumeona ni mfano tu, Tazara peke yake inadaiwa bilioni 1.9, Tanganyika parkers nayo bilioni 1.4 kwa Mkoa wa mbeya
Taasisi za Serikali zinadaiwa bilioni 5.4 hizi ni hela nyingi sana hivyo Wizara fuatilieni haya madeni" Alisema Mhe. Dkt. Aloyce Kwezi.

Mhe.Dkt.Aloyce Kwezi aliongeza kwamba Wizara inabidi ilete orodha kwa kamati ya wadaiwa wote wakubwa wote wanaodaiwa na Wizara ya Ardhi pamoja na
Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kwa upande wake Mhe.Angelina Mabula Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alishukuru uongozi wa Mkoa wa mbeya kwa ushirikiano mzuri walioonyesha toka wamefika na aliahidi kuleta orodha ya wadeni wote kwa kamati ya Bunge.

Pia Mhe. Mabula alilipongeza Jiji la Mbeya kwa kazi nzuri na kusisitiza zipo Halmashauri zingine ambazo zimerejesha hela kwa wakati ambazo ni Kahama, Ilemela, Geita, ataufanyia kazi ushauri wa kamati wa kukopeshwa tena wanaofanya vizuri..

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament