Parliament of Tanzania

Bunge lapitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20

Bunge limeridhia na kupitisha Bajeti kuu ya nne ya serikali ya awamu tano kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Bajeti hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 33.1. imepitishwa asilimia 78.2 ya Wabunge baada ya mjadala wa siku saba (7).

Akitoa matokeo ya kura, Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai amesema jumla ya Wabunge waliopiga kura ni 380, huku Wabunge ambao hawakuwepo ni 12 na hakuna Mbunge ambaye hakupiga kura.

Jumla ya wabunge 297 ambao ni sawa na asilimia 78.2 walipiga kura za ndiyo ishara ya kukubali makadirio ya matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Kwa upande mwingine wabunge waliopiga kura za hapana ni 83 sawa na asilimia 21.8 ya Wabunge waliopiga kura.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2019/20

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's