United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Bunge ni Chombo cha uwakilishi wa Wananchi kama Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyotumika:
“Kutakuwa
na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na
Wabunge. Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekelezza yote aliyokabidhiwa na
katiba hii. Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya
Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na
kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika
utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii”
Kimsingi,
Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi. Kwa kuwa haiwezekani wananchi wote
kukusanyika mahali pamoja na kufanya maamuzi muhimu katika uendeshaji wan chi,
uwakilishi hauna budi kuwepo. Hii inamaanisha kwamba Wabunge wanapokuwa Bungeni
hutekeleza majukumu yao kwa niaba ya wananchi.
Ofisi
ya Bunge, kwa kutambua hilo imeweka utaratibu ambapo jamii huruhusiwa
kushuhudia namna ambavyo wawakilishi wa wananchi wanavyotekeleza majukumu yao.
Wageni Bungeni
Bunge hufanya mikutano yake mara nne kwa
mwaka mjini Dodoma. Wakati wa mikutano hiyo, watu mbali mbali huruhusiwa
kutembelea Bunge na kujionea jinsi linavyoendesha shughuli zake. Kanuni ya 136
(1) ya Kanuni za kudumu za Bunge inaeleza ifuatavyo:
“Wageni wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi wa Mikutano ya
Bunge katika sehemu yoyote ya Ukumbi
huo ambayo itatengwa kwa ajili yao”
Utaratibu wa kutembelea Bunge upo wazi ambapo
watu binafsi, Vikundi, watumishi wa Taasisi za Serikali, Mabalozi
wanaowakilisha mataifa yao nchini, Mashirika ya Kidini, Asasi za Kiraia,
Taasisi za Kijamii, Wanafunzi (Shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya
Elimu ya Juu) na Wageni kutoka Mabunge nje ya Tanzania au Taasisi za Kimataifa
hutumia fursa iliyopo kutembelea Bunge
na kuona jinsi linavyoendesha shughuli zake.
Utaratibu wa Kufuatwa
Utaratibu mzuri unaopaswa kufuatwa na
wanaotaka kutembelea Bunge ni kuandika barua ya maombi ya kutembelea Bunge.
Barua hiyo ni vyema ikaeleza tarehe inayokusudiwa, idadi na madhumuni ya
kutembelea Bunge na kutumwa kwa anwani ifuatayo:
Katibu wa Bunge
S.L.P 941
DODOMA
Au
Katibu wa Bunge
S.L.P 9133
DAR ES SALAAM
Ofisi ya Bunge hujibu barua zote za maombi ya
kutembelea Bunge. Maombi yote yatakayozingatia utaratibu hukubaliwa kama
yalivyo, isipokuwa tu kama maombi mengi yamegongana tarehe na idadi ya watu ni
kubwa kuzidi uwezo wa maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya wageni. Ikitokea
hivyo, ushauri hutolewa kwa baadhi ya waombaji kupanga tarehe nyingine muafaka.
Ukaaji ndani ya Bunge
Kanuni ya 140 ya Kanuni za kudumu za Bunge
inaelekeza kuwa, Spika ataweka utaratibu maalumu wa Ukaaji wa Wabunge ndani ya
Bunge bila Kuathiri mpangilio ufuatao:
Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Special Seats (CHADEMA)