Parliament of Tanzania

Naibu Spika akutana na kuzungumza na Spika wa Jimbo la Shanghai la nchini China

Spika wa bunge la Shengai Yin Yicui,pamoja na Wajumbe kumi na mbili wa Bunge hilo wamekutana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa lengo la kubadilishana uzoefu mbalimbali kwa pande zote mbili.

Spika Yin Yicui na wenzake wamefurahishwa na mapokezi na kusema kuwa baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Tanzania wakati alipotembelea Shengai, walifurahia kupata mwaliko huo na kuahidi kuja Tanzania.

Spika huyo aliongeza kuwa Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai limekuwa na uhusiano mzuri toka huko nyuma na kulenga kuendeleza maslahi mapana ya maendeleo ya Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai.

Mazungumzo baina yalijikita katika kuona jinsi wanavyoweza kushirikiana katika sekta ya elimu,mazingira na utunzaji wa maliasili na wanyamapori.

Kwa upande wa mazingira, Bunge la Shengai linaangalia namna linavyoweza kusaidia uboreshaji wa mazingira, ambapo walipongeza serikali ya Tanzania kwa kupitisha sheria ya kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki na kuongeza kuwa, nchini kwao jimbo la Shengai wanajiandaa kupitisha sheria ambayo inahitaji utenganishi wa aina za takataka za majumbani.

Naibu Spika alimshukuru jinsi China wanavyoisaidia Tanzania kwa upande wa ufadhili wa masomo ya nje wanafunzi wanaotoka Tanzania, ambapo alisema ufadhili wao ni tofauti na ufadhili wa nchi nyingine, kwamba China huomba wanafunzi kwenda kusoma China wakati mataifa mengine wanafunzi huomba moja kwa moja katika nchi wanazopenda kusoma, pia katika vyuo vya VETA wataangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na Tanzania ikiwemo kusaidia vifaa vya kufundishia kama vile kompyuta

Mwisho walizungumzia namna ya Tanzania kutunza raslimali zilizopo nchini ambapo ni pamoja na wanyamapori na uoto wa asili, na kuahidi kuwa bega kwa bega na Tanzania ili kukuza na kuendeleza rasilimali za nchi.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's