Parliament of Tanzania

Katibu wa Bunge awapongeza Watumishi wa Ofisi ya Bunge

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi, ndc amewapongeza wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge kwa utendaji kazi wao mzuri wa majukumu yao.

Bi Nenelwa alitoa pongezi hizo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Bunge kinachofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Zanzibar.

“Napenda nichukue fursa hii kuwapongeza sana wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, tunafanya kazi kwa bidii bila kuchoka ili kutimiza majukumu yetu, changamoto ni za kawaida lakini utendaji kazi wetu ni mzuri,” alisema.

Alitumia fursa hiyo pia kuwashukuru watumishi wote waliomtakia kheri kwa kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha.

“Wote kwa pamoja tuendelee kushirikiana maana tunajenga nyumba moja, kama kuna mtu atakuwa na ushauri wowote wa kujenga anakaribishwa,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Bajeti, Ndugu Michael Kadebe akiwasilisha Taarifa Utekelezaji wa Bajeti ya Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 alisema Mfuko wa Bunge katika mwaka huo wa fedha umetekeleza majukumu yake kama yalivyopangwa na kwa kuzingatia Kanuni, Taratibu, Sheria na Mifumo ya Fedha iliyopo.

Akiwasilisha mada kuhusu Maendeleo ya Watumishi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Jane Kajiru alisema Idar itaendelea kushuhulikia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya watumishi.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Prof. Kitila Alexander Mkumbo

Ubungo (CCM)

Contributions (2)

Profile

Hon. Asya Sharif Omar

Special Seats (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Kilumbe Shabani Ng'enda

Kigoma Mjini (CCM)

Contributions (2)

Profile

View All MP's