Parliament of Tanzania

BUNGE LAAHIRISHWA HADI NOVEMBA 5, 2019

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ameahirisha Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge hadi tarehe 5, Novemba 2019.

Akizungumza kabla ya kuahirisha Bunge, Mhe. Spika aliwatakia heri wabunge wakati huu ambapo wanarudi majimboni kutekeleza majukumu yao ya kibunge.

“Napenda kuwatakia kila la kheri wakati huu mnaporudi majimboni, kuweni makini na vyombo vyenu vya usafiri nendeni taratibu,” alisema.

Awali akisoma Hotuba ya kuahirisha Bunge, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa aliwapongeza viongozi wote wa Bunge kwa kuendesha Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge kwa ufanisi.

Pamoja na mambo mengine vilevile, Mhe. Waziri Mkuu alizungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo amewataka wadau watakaoshiriki katika uchaguzi huo kujiepusha na vitendo vya rushwa na uvunjifu wa amani.

Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua pale itakapothibitika vitendo hivyo kufanyika huku akiwataka Watanzania wote wenye sifa wajiandikishe katika orodha ya wapiga kura, wachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki kupiga kura kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Ahmed Mabukhut Shabiby

Gairo (CCM)

Contributions (14)

Profile

Hon. Sadifa Juma Khamis

Donge (CCM)

Contributions (2)

Profile

View All MP's