Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kuiwekea SUMA JKT mazingira rafiki ili iweze kukopa na kutekeleza miradi yake kwa wakati?

Supplementary Question 1

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa naomba kuuliza Serikali, je, iko tayari kuwa na mpango mahsusi wa kuisadia SUMA JKT katika kuhakikisha kwamba tunajitosheleza katika suala zima la chakula na mafuta ya kula? Mipango mahsusi? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Chumi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo tayari kuangalia vipengele mahsusi vya kusaidia mashirika yake na mashirika mengine, lakini ushauri wake pia tumeuchukua na tunaenda kuufanyia kazi.