Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itashawishi mabenki kufungua benki nchini Congo DRC katika Miji ya Kalemie na Uvira ili kurahisisha biashara?

Supplementary Question 1

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Kalemie na Uvira ni miji ambayo iko karibu sana na Mikoa ya Kigoma, Katavi na Sumbawanga: Je, Serikali haioni haja ya kufanya haraka kuhakikisha kwamba maeneo haya ya Uvira na Kalemie yamefunguliwa hizo branches za CRDB? Ahsante. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nashon William Bidyanguze, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli Serikali imeona haja hiyo na ndiyo maana kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, kwamba Benki Kuu ya Tanzania ilishatoa kibali kwa CRDB sasa, lakini tumetoa wito kwa benki nyingine zote nchini ambazo ziko tayari kuwekeza katika miji hiyo ya Congo, basi Serikali imetoa idhini ya kufanya zoezi hilo. (Makofi)