Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme katika Vijiji vya Chemba?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Katika mpango huo vipo vijiji vinne ambavyo havikuwekwa kwenye mpango, sijui sababu ni nini. Vijiji hivyo ni Kelemakuu, Birise, Muungano na Sankaleti. Nataka kujua, Serikali ina mpango gani sasa wa kuviingiza vijiji hivyo kwenye mpango wa REA? Ahsante.

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Monni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vijiji hivyo vinne vya Kilemakuu pamoja na vingine vyote vipo katika hivyo vijiji 12 ambavyo vimebakia katika utekelezaji wa mradi na kufikia hiyo tarehe 31 Oktoba vitakuwa pia vimewashiwa umeme. (Makofi)

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme katika Vijiji vya Chemba?

Supplementary Question 2

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Usimikaji wa nguzo katika Kata ya Likawage na Vijiji vyake vya Nainoku, Liwiti na Likawage yenyewe katika Jimbo la Kilwa Kusini umekwama kutokana na changamoto ya TFS kuzuia kupitisha nguzo katika eneo la hifadhi. Je, ni nini mpango wa Serikali wa kushirikiana kati ya Wizara ya Nishati na Wizara ya Maliasili na Utalii kuondoa utata huu?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kassinge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, awali kulikuwa kuna changamoto kubwa ya Sheria ya TFS ambayo ilikuwa inatutaka sisi Wizara ya Nishati au watumiaji wengine wa maeneo yao kulipia gharama fulani lakini baada ya majadiliano tumekubaliana kwamba, kwa sababu tunafanya miradi ya Serikali kwa pamoja basi tupeane hizi leeway kwa ajili ya kupitisha hii miundombinu. Kwa hiyo, case by case zikitokea tunazi-solve kulingana na maeneo husika. Nitawasiliana na Mheshimiwa Mbunge ili tuone wapi tulipokwama na tuweze kutatua tatizo hili kwa sababu maeneo mengine tayari tumelimaliza.

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme katika Vijiji vya Chemba?

Supplementary Question 3

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kumekuwa na changamoto kubwa ya kurukwarukwa kwa kuwekewa umeme kwa wananchi katika Kata za Kalunde na Ndevelwa katika Jimbo la Tabora Mjini. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawekea wananchi wote umeme kwa usawa ili waweze kunufaika na huduma hii? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba hatujaweza kama Serikali kuwa na uwezo wa kumuunganishia kila mwananchi anayehitaji umeme leo, lakini mpango mkubwa wa Serikali ni kutafuta shilingi takribani trilioni sita na bilioni kama mia tano ambazo zitafikisha umeme kila kitongoji katika nchi hii, kila mtaa katika nchi hii. Hivyo, tunaamini wananchi walio wengi kwenye maeneo hayo wataweza kuupata umeme kwa wakati mmoja. Kwa sasa, kwenye mradi tuliokuwa nao wa REA III round II, tunaenda na wananchi wachache kama sampling kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mradi umeanza, lakini tunaendelea kuongeza kuwafikia wananchi wengine kwa kadri ya uongezekaji wa bajeti.

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme katika Vijiji vya Chemba?

Supplementary Question 4

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Wananchi wa Kijiji cha Nyabikurungo Kata ya Ukuraijo waliwekewa nguzo na baadaye zikaondolewa bila kuunganishiwa umeme lakini pia Kijiji cha Bugaza, Kata ya Kimuli. Nataka kujua ni lini hawa wananchi watawashiwa umeme katika hayo maeneo?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba programu yetu ya kupeleka umeme vijijini itakamilika mwezi Disemba mwaka huu. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba kijiji hicho pia kitapata hiyo nishati ya umeme na mkandarasi anayepeleka umeme wa Rukomi na Kawahya tutamsimamia ili aweze kufanya kazi hiyo kwenye maeneo hayo.