Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Kombo Hamad

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. JUMA KOMBO HAMAD aliuliza:- Ni muda mrefu sasa Kikosi cha Polisi Marine Pemba hakina boti ya doria hali inayopelekea polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku. (a) Je, Serikali inatambua hilo? (b) Kama inalitambua, je, ni lini Serikali itakipatia Kikosi cha Polisi Marine Pemba boti za doria ili kuwawezesha polisi hao kufanya kazi zao kwa ufanisi?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Spika, ni kawaida kwa Wizara hii ya Mambo ya Ndani kila siku kuja na jawabu lilelile. Swali langu la mwanzo ni kukosekana kwa boti ya doria katika Kisiwa cha Pemba na mazingira ya jiografia yalivyo ya Kisiwa cha Pemba ni hatari kwa mazingira yela yalivyo; je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba kuwakosesha wanamaji hawa wa boti ya doria ni kuhatarisha mazingira ya amani kwa nchi yetu hii ya Tanzania?
Swali la pili, kimsingi Wizara ya Mambo ya Ndani imekuwa ikitenga bajeti ya lita kadhaa za mafuta yasiyopungua 1200 kila mwezi je, Mheshimiwa Waziri anaweza kutueleza mafuta haya yanatumikaje ukizingatia kwamba ndani ya Kisiwa cha Pemba hakuna boti ya doria kwa Kikosi cha Wanamaji? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu katika swali la msingi kwamba wakati jitihada za kupeleka boti Pemba pale uwezo utakapopatikana linaendelea kwa sasa hivi tunafanya kazi kwa mashirikiano mazuri na vikosi vingine mbalimbali kama vile vikosi vya SMZ ambavyo wana boti za doria zinazokidhi mahitaji kwa kipindi hiki kutoa huduma maeneo ya Pemba ikiwemo Jimbo la Wingwi.
Mheshimiwa Spika, lakini kuhusiana na mafuta kimsingi ni kwamba fedha kwa ajili ya matumizi ya mafuta ya Jeshi la polisi kiujumla hazitoshi kwa hiyo, ningedhani kwamba Mheshimiwa Mbunge badala ya kuhoji matumizi angehoji uwezekano wa kuongeza kwa sababu hata zilizopo hazikidhi mahitaji ya huduma katika matumizi ya Jeshi la Polisi.