Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Kalebe – Bukoba Vijijini ili kuwezesha magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kupita kwenye daraja hilo?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; daraja hili ni la muda mrefu sana mimi napenda Serikali itueleze uhimilivu wa daraja hili ni wa kiwango kipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Serikali kutojenga daraja hili ni kuendelea kuwapa adha wasafirishaji wanaosafirisha mizigo zaidi ya tani 10 ambao wanalazimisha kufanya mzunguko kupitia barabara ya Kyaka kwenda mpaka Bukoba Manispaa.

Je, hawaoni kwamba wanaendelea kuwapa adha wasafirishaji hawa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, daraja alilolitaja la Kalebe tunavyoongea sasa hivi mkandarasi yupo anafanya kazi na tunategemea akamilishe mwezi Oktoba japo kwa jinsi anavyokwenda anaweza akamaliza hata kabla. Lengo kuu la kufanya usanifu huu upya ni ili daraja hili liweze kubeba mizigo zaidi ya tani 10 kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera na yapo madaraja mengine pia tunafanya usanifu ili kuyapa uwezo zaidi wa kubeba mizigo tofauti na ilivyo sasa. Ahsante.