Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vedasto Edgar Ngombale Mwiru

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE aliuliza:- Serikali katika awamu zote imekuwa ikiweka kipaumbele katika sekta ya Kilimo na Mifugo kwa umuhimu wake kwa maendeleo ya wananchi katika nchi yetu, lakini Wilaya ya Kilwa kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi yetu, imekuwa na migogoro inayotishia amani kati ya wakulima na wafugaji katika baadhi ya Vijiji vikiwemo vya Ngea, Kinjumbi, Somanga, Njianne, Namandungutungu na Matandu, kutokana na wafugaji kupitisha, kulisha, kunywesha na kuharibu mazingira katika mashamba ya wakulima na Hifadhi ya Misitu ya Vijiji kama Msitu wa Likonde, Mitarute na Bwawa la Maliwe katika Kijiji cha Ngea, ambacho hakipo katika mpango wa kupokea wafugaji:- Je, Serikali inatoa wito gani kwa wafugaji wanaoruhusu mifugo yao kuwatia hasara na njaa wakulima na kuharibu mazingira ya baadhi, ili kuepusha uvunjifu wa amani ambao unaweza kutokea wakati wowote kuanzia sasa?

Supplementary Question 1

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini siyo kweli kwamba katika Wilaya ya Kilwa kuna wakulima wanaingilia maeneo ya wafugaji na kama hivyo ndivyo, Mheshimiwa Waziri anao uwezo wa kunitajia vijiji vitano ambavyo kuna migogoro ya wakulima kuingilia maeneo ya wafugaji, hiyo ni moja.
Mbili, kwa kuwa, mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Kijiji cha Ngea haukutenga eneo kwa ajili ya wafugaji na kwa kuwa, Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Ngea, ulishaamua wafugaji waondoke na kupata baraka za uongozi wa Wilaya. Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana na mimi kwenda kuona athari ambazo wakulima wamezipata lakini athari za hifadhi za misitu pamoja na Bwawa la Maliwe?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kusema kwamba hizi ni taarifa ambazo tumezipata, nikuhakikishie ndugu yangu Ngombale mimi niko tayari kwanza kufika Kilwa. Katika sehemu yako na pili naomba nikuhakikishie kwamba, nitafika Kilwa, siyo kwa ajenda hii tu ya wakulima na wafugaji peke yake hapana! Kuna mambo mengi ya kimsingi ya kuweza kuyafuatilia kule Kilwa ambapo ofisi yangu ina kila jukumu la kufanya hivyo ili wananchi waweze kupata huduma.
Mheshimiwa Spika, lakini suala zima la vijiji nikutaarifu kwamba, katika miaka ya nyuma kulikuwa na Mkuu mmoja wa Wilaya pale alikuwa anaitwa Nurdin Babu, katika hiki Kijiji cha Ngea ulichokizungumza japokuwa mwanzo wafugaji walikataliwa lakini baadaye Mkuu wa Wilaya alipokwenda kufuatilia baadhi ya wananchi walisema hapana, tunahitaji wafugaji waendelee kuwepo.
Kwa hiyo, kwanza kuna changamoto kidogo katika maeneo yetu, lakini kubwa zaidi haya yanatokea ni nini mara nyingi sana wakati mwingine hata hawa Viongozi wetu wa Vijiji inakuwa ni tatizo, mwanzo wafugaji walikataliwa walipoingia pale, lakini baada ya kukaa muda fulani tayari sasa kukawa na mgogoro mpaka Mkuu wa Wilaya pale aliingia site na wananchi wamesema bwana sisi hapa hatuna matatizo kwa sababu wafugaji wamechimba kisima hapa, sisi tunaishi vizuri, Mkuu wa Wilaya nenda, leo hii suala hili limekuja! Hata hivyo, nimesema ngoja niyachukue haya kwa sababu lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanaishi katika hali ya usalama. Hii migogoro mwisho wa siku inahatarisha maisha ya wananchi wetu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, hivyo nayafanyia kazi ndugu yangu, wala usipate hofu.