Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwasaidia Wananchi wa Mwera ambao hawakuingizwa TASAF na wanaishi chini ya viwango vya umaskini?

Supplementary Question 1

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ningeomba Serikali itusaidie kufahamu.

Je, kwa wale ambao walikuwemo kwenye mfuko wa TASAF lakini hawaku–qualify kuondoka lakini hawakurudishwa tena kwenye mfuko huu kwenye muda huu? Tafadhali.

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zahor Haji, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa walengwa ambao walikuwemo kwenye mpango wa TASAF lakini baadae ikaonekana hali zao zimeimarika na kutolewa haijazuiwa wao kurudishwa kwenye mpango wa TASAF pale ambapo watakuwa wameshuka chini ya vile vigezo ambavyo vimewekwa vya mtu kuonekana ana hali nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninaomba nitakaa na Mheshimiwa Zahor Haji ili tuweze kuona ni namna gani wataalamu wetu wa TASAF wanaweza kwenda pale Mwera na kuangalia hizo kaya ambazo zilitolewa na ziweze kurudi katika mpango wa TASAF.