Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Santiel Eric Kirumba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SANTIEL E. KIRUMBA aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kujenga vyoo maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika madarasa mapya yanayojengwa ili wanafunzi hawa wasikose masomo pindi wanapokuwa kwenye siku zao?

Supplementary Question 1

MHE. SANTIEL E. KIRUMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali; nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na watoto wengi wa kike kukosa masomo siku tano mpaka saba kwa hiyo kunasababisha kwa mwaka kukosa masomo kwa siku 50. Nini commitment ya Serikali katika madarasa haya mengi mapya ambayo hayana mfumo huu wa vyumba maalum?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Santiel Erick Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ameianisha hiyo changamoto, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi Ofisi ya Rais – TAMISEMI tunazielekeza halmashauri zote sasa kujenga vyumba ambavyo vinaweza vikawasaidia watoto wa kike kujistiri wakati wa hedhi. Lengo ni kuhakikisha kwamba Watoto hawa hawakosi masomo wanapokuwa katika kipindi chao ili kuweza kuwasaidia kama ambavyo katika michoro yetu mipya ambayo tumeianisha.