Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: - Je, ni hatua gani zitachukuliwa kwa walipa kodi walioshindwa kulipa na kuwa na malimbikizo makubwa lakini wapo tayari kulipa?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili. Kwanza nashukuru kwa majibu.

Je, ni lini zoezi hili litakamilika ukizingatia umuhimu wa kukusanya kodi na kwa vile ni muda tangu Mheshimiwa Rais alipotoa agizo hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali na TRA ina mkakati gani rafiki wa kufanya makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara yanayoendana na mapato halisi ili kuzuia wafanyabiashara wasishindwe kulipa kodi hizi? Ahsante sana.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali kwanza, inategemea ushirikiano ya mteja wakati wa kufanya majadiliano. Kama mteja atakuwa na ushirikiano mzuri basi suala hili linamalizika kwa kipindi kifupi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili; mikakati ambayo tumechukua sisi Serikali ni kutoa fursa kwa wateja, yaani wafanyabiashara, kufanya self assessment, yaani kujifanyia tathmini wenyewe halafu na sisi tunajiridhisha. Mkakati wa pili ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara wote ili wafate taratibu za kulipa kodi.