Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: - Je, lini minara ya mawasiliano itajengwa katika Kata za Endanywish, Endagulda, Gidurdagaw, Yaeda Ampa, Hayeda na Endanilay?

Supplementary Question 1

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante nampongeza kwanza Mheshimiwa Waziri kwa kusoma vizuri vijiji hivyo, lakini kuna mnara ambao uko Masqaroda haujawaka mpaka leo na umejengwa kwa gharama kubwa.

Je, lini Mheshimiwa Waziri mnara huu utapata kuwaka ili mawasiliano yakapatikana Jimbo la Mbulu Vijijini?

Pamoja na majibu yako haya na kata ulizotaja na kwa kuwa hakuna uhalisia wa kutosha; je, uko tayari kufuatana na mimi kwenda Jimboni ukayaona haya yote uliyoyasema na majibu yako haya? (Makofi)

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Massay Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba mnara alioutaja umejengwa na umekamilika kwa maana ya vifaa, lakini ulikuwa haujawashwa kwa sababu tulikuwa na changamoto ya vifaa vya mwisho vya kuwashia ule mnara kutokana na tatizo la covid uzalishaji wa baadhi ya vifaa ulichelewa, lakini sasa vifaa vipo tayari na mnara huu utakwenda kuwashwa.

Mheshimiwa Spika, pia niko tayari kuambatana naye tumekuwa tukishirikiana naye katika kutatua tatizo la mawasiliano katika eneo lake; na yeye anajua kwamba hata katika mradi wa kidijitali tumeweka zaidi ya minara saba kwenye Jimbo lake kwa ajili ya ku-facilitate mawasiliano. (Makofi)

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: - Je, lini minara ya mawasiliano itajengwa katika Kata za Endanywish, Endagulda, Gidurdagaw, Yaeda Ampa, Hayeda na Endanilay?

Supplementary Question 2

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kunipa nafasi. Kijiji cha Uliwa kata ya Uhungilo kijiji ambacho kina shule, kina sekondari, kina zahanati lakini hakina mawasiliano kabisa ya aina yoyote, ni lini sasa Serikali itapeleka mawasiliano katika kijiji hicho cha Uliwa?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Mwanyika kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli maeneo aliyoyataja ni katika orodha tuliyowasilisha hapa Bungeni katika ile miradi 763 ya Tanzania ya kidijitali, maeneo aliyoyataja baadhi yake yamo na nimuahidi kwamba tutakapotangaza miradi hiyo basi ujenzi utaanza mara moja. (Makofi)