Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuongeza maduka ya kutolea dawa kwa kutumia Bima ya Afya ili kuondoa usumbufu wanaopata wananchi wa Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante; kwa kuwa kuna ucheleweshaji mkubwa wa malipo ya watu wanaomiliki maduka hayo na hospitali.

Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuweka njia nzuri ya kuwafanya wamiliki wa maduka yale waweze ku-invest au kuingia katika uwekezaji huu wa kutoa huduma?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mfumo uliokuwepo kabla wa kuandika karatasi na kujaza fomu za kawaida umekuwa ukichelewesha hayo malipo ambayo imekuwa ni sababu mojawapo ya wamiliki wengi wa vituo na maduka kusita kujiunga na Bima ya Afya, lakini sasa bima ya afya imeshatengeneza mfumo mtandao ambapo sasa malipo hayo yanaweza moja kwa moja yakaingizwa kwenye mtandao siku hiyo na akaweza kulipa mapema kila baada ya mwisho wa mwezi.

Kwa hiyo, tunaielekeza Bima ya Afya sasa waweze kufikisha hiyo huduma Zanzibar mara moja ili hilo tatizo liweze kuondolewa. (Makofi)