Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Primary Question

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wakulima wa mazao ya viungo kama Iliki, mdalasini, pilipili manga na karafuu wa Kata ya Kigongoi, Mhindano na Bosho Wilayani Mkinga ili waweze kuongeza uzalishaji wa thamani ya mazao hayo?

Supplementary Question 1

MHE. DUSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tija ya kilimo katika mazao haya ipo chini sana kwa sababu ya mbegu duni: Nini kauli ya Serikali katika kuwasaidia wakulima hawa kupata mbegu bora ili kuweza kuongeza tija katika kilimo chao?

Pili, Serikali iko tayari kushirikiana na Mkoa wa Tanga katika kuboresha mnyororo wa thamani wa kilimo cha mazao haya?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kitandula kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikiri, kama nchi kwa muda mrefu tulikuwa hatujayapa kipaumbele mazao haya ya viungo. Nataka tu nilihakikishie Bunge lako tukufu, kwamba kwanza tumeya-cluster kama sehemu ya mazao ya horticulture, kwa hiyo, yatasimamiwa kwa karibu na idara inayohusika na mazao haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tumekiagiza kituo chetu cha Mliongano kwamba kianze kufanya kazi ya utafiti na uzalishaji wa mbegu na miche kwa ajili ya mazao ya Hiliki na mazao ya viungo pamoja na mazao ya matunda ya machungwa ambayo yanalimwa kwa wingi katika Mkoa wa Tanga ili kuondoa matatizo yanayowakabili wakulima wetu na kuyapa center stage mazao haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kushirikiana na mkoa, nataka tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tuko tayari kama Wizara ya Kilimo kukaa nao ili tujadiliane ni namna gani tunaweza kuwasaidia wakulima hawa wadogo kwenye value chain ya mazao kama ambavyo tumeamua kuwasaidia wakulima wa mkonge kwa kuwapatia makorona; na Bodi ya Mkonge itanunua makorona matatu kwa ajili ya kuwapa wakulima wadogo wa maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama Wizara tuko tayari kukaa nao. (Makofi)