Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohammed Maulid Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiembesamaki

Primary Question

MHE. MOHAMED MAULID ALI aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kujikita zaidi kwenye uchimbaji wa Malambo ya kuhifadhia maji ya mvua na kujenga mabomba ya kuchukua maji toka kwenye maziwa na mito yote kuliko kuendelea kutumia gharama kubwa za kuchimba visima bila mafanikio?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMMED MAULID ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nilitaka kumwuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mpango gani wa Serikali katika bajeti ijayo kuhusu suala zima la kutoa maji kwenye maziwa na kupeleka kwa wananchi? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mohamed Maulid Ali kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Wizara, nimesema katika jibu langu la msingi, ni kuona kwamba tunakwenda kutumia vyanzo vya uhakika, ikiwemo maji ya maziwa makuu. Hivyo tuko kwenye mpango huo, lazima tutatekeleza. (Makofi)