Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nancy Hassan Nyalusi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Igowole – Nyigo kilomita 54 ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025?

Supplementary Question 1

MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, katika ukanda huu kuna barabara tatu ambazo ni Gohole, Nyigu, Mtwango, Nyololo na Mafinga Mgololo.

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba barabara hizo zitapitika katika kipindi hiki cha mvua ambazo zinaanza? Kwa sababu hazipitiki. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nancy Nyalusi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba eneo hili Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ameshaji-commit. Tulikubaliana kwamba mwaka wa fedha unaofuata 2022/2023 tutaanza kujenga eneo hili kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili naomba nitumie nafasi hii kutoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa, atembelee maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja. Afanye tathmini na kama kuna shida basi matengenezo yafanyike, wananchi wapate huduma ya usafiri wa miundombinu wakati wote wa mvua. Ahsante.