Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kusamehe kodi za miaka ya nyuma taasisi za dini 7 zilizokuwa zikiendeshwa kwa utaratibu usiolenga kupata faida na kuziwekea utaratibu taasisi hizo kuanza kulipa tangu walipojulishwa kutakiwa kulipa kodi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri na nampongeza Waziri kwa kutoa majibu haya ambayo yanatoa faraja sana kwa hawa wanaoendesha shughuli hizo. Hata hivyo, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, Serikali itakuwa tayari kurejesha kodi iliyokusanywa kutoka kwenye taasisi hizo kwa shinikizo na hatimaye kuzidhoofisha sana?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali iko tayari kuchukua hatua za kinidhamu kwa hawa maafisa wa TRA wanaokiuka sheria? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, Serikali ina utaratibu wa kurejesha fedha ambazo zilichukuliwa na kwa mujibu wa sheria zinatakiwa kurejeshwa kwa utaratibu ulio wa kawaida wa kufanya refund na refunds hizo huwa zinafanyika kwa mujibu wa sheria. Kwa maeneo ambako kuna makosa ya ukiukwaji wa kisheria, taratibu za kisheria huwa zinafuatwa na hatua stahiki za kinidhamu kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka sheria.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama kuna maeneo ambako maafisa wetu wamekiuka sheria, taratibu za kisheria zitafuatwa na hatua za kisheria kuweza kuchukuliwa.