Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kujenga Barabara ya Kijiji cha Uzena kwenda Kijiji cha Njomlole katika Jimbo la Mbinga Mjini kwa kiwango cha changarawe ili iweze kupitika kwa wakati wote?

Supplementary Question 1

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza. Barabara hiyo ili iweze kukamilika inatakiwa yajengwe madaraja mawili; je, Serikali haioni kwamba kiasi cha fedha cha shilingi milioni 10 kilichotengwa hakitatosheleza kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameuliza, kwa nini Serikali isijenge pamoja na daraja lingine kwa sababu hiyo barabara ina madaraja mawili na fedha tuliyotenga ni ndogo kukamilisha hiyo barabara. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda kufanya tathmini na baada ya hiyo tathmini tutatafuta fedha ili tuweze kumalizia na hilo daraja lingine ili liweze kukamilika. Ahsante sana.