Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAS G. NGASSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipatia Hospitali ya Wilaya ya Igunga gari la kubebea wagonjwa kwa kuwa lililopo limechakaa sana?

Supplementary Question 1

MHE. NICHOLAS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Sasa naomba kuuliza swali la nyongeza kwa Serikali, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, Sura ya 7 imeweka vigezo kwa Hospitali za Kata na Wilaya na moja ya kigezo ni lazima kuwe na gari la wagonjwa. Sasa Serikali imechukua gari la Kituo cha Afya cha Choma imepeleka Igunga na Kituo cha Afya cha Choma tena kimekosa gari. Je, Serikali haioni tunaendelea kukanyanga Sera ambayo tumejitungia sisi wenyewe? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nicholas Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, gari la Kituo cha Afya cha Choma limepelekwa katika Hospitali ya Halmashauri ili kuweza kuboresha zaidi huduma za Halmashauri kwa kuwa Hospitali ya Halmashauri ina wagonjwa wengi zaidi kuliko Kituo cha Afya. Hata hivyo, gari hilo linafanya kazi katika vituo vyote viwili kwa maana Kituo cha Afya na Hospitali ya Halmashauri.