Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. David Mathayo David

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Same Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. DAVID M. DAVID Aliuliza:- Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi huchangia Pato la Taifa kutokana na shughuli za utalii. Je, Serikali haioni kuwa umefika wakati wa kuukarabati Uwanja wa Ndege wa Same Mjini ili ndege ndogo na za kati ziweze kutua kuleta watalii wa ndani na nje ya nchi katika Hifadhi ya Mkomazi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Naibu Spika, ninadhani kwamba majibu haya kidogo sijaridhika sana, lakini niseme ni mwanzo.

Mheshimiwa Naibu Spika, faru weusi pamoja na wanyama wengine wanapatikana katika Hifadhi za Taifa tatu tu katika nchi hii zikiwemo Serengeti, Ngorongoro pamoja na Hifadhi ya Mkomazi. Upande wa Kenya wana kiwanja cha ndege pale Tsavo, upande wa Kenya Hifadhi ya Tsavo ndiyo inayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, na hivyo wanapata watalii wengi kwa sababu wao wana kiwanja cha ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile umbali wa kutoka Arusha na KIA ni mkubwa sana ukizingatia na uhitaji wa watalii kuja kuona faru weusi walioko kwenye sanctuary pale Mkomazi National Park. (Makofi)

Ninaomba Serikali iangalie uwezekano wa kukarabati Uwanja wa Ndege wa Same ili watalii hao waweze kufika kwa urahisi na kuongeza Pato la Taifa kama Mheshimiwa Rais alivyosema jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, ninaomba inapowezekana Mheshimiwa Waziri aje pale Same ili aweze kuona mazingira hayo ninayozungumzia, kwamba uwanja upo unahitaji marekebisho ili tuweze kukuza uchumi kupitia utalii. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuleta wazo zuri sana ambalo kimsingi siyo la Same Magharibi peke yake, hili ni jambo la Kitaifa.

Ninaomba nitumie nafasi hii kumuelekeza Katibu Mkuu Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, awatume wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege waende Same Magharibi wafanye tathmini, tuangalie cost implication ili kiwanja hiki kikarabatiwe mapema iwezekanavyo, fedha itakapopatikana kupitia watalii katika eneo hili itasaidia kuboresha hotuba nzuri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya jana ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili; naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayari kabla Bunge hili halijaisha naomba kibali cha Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa Waziri Mkuu, twende Sa me kwa sababu kuona ni kuamini, tushuhudie hali halisi na tuongeze maelekezo ya ziada. Ahsante. (Makofi)