Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY (K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY) Aliuliza:- Mwaka 2015 Serikali ilitangaza kugawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupitia vikao vya Mabaraza ya Madiwani wa Halmashauri za Mbulu Wilaya na Mbulu Mji walipitisha rasmi mgawanyo wa rasilimali na madeni. Je, ni lini Serikali itarejesha tamko la mapendekezo hayo ili kufanikisha maendeleo ya mambo yaliyopendekezwa?

Supplementary Question 1

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninalo swali la nyongeza.

Kwa kuwa asilimia hizi zipo kisheria na bado kuna ukakasi katika mgawanyo huu; je, yupo tayari sasa kuja kuona uhalisia wa suala lenyewe katika Jimbo la Mbulu Mji na Vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE):
Mheshimiwa Naibu Spika, niko tayari kushirikiana naye na Halmashauri ya Mbulu kuweza kuona namna gani tunatatua huo ukakasi ambao Mheshimiwa Mbunge ameuripoti uliotokana na mgawanyo wa mali kati ya Halmashauri ya Mbulu Vijijini na Halmashauri ya Mbulu Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie kwamba baada ya Mkutano huu wa Bunge tutapanga tuone utaratibu mzuri wa kuwaza kutatua changamoto hiyo. (Makofi)