Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMAR M. KIGUA aliuliza:- Ulipaji kodi ni chanzo kikuu cha mapato ya nchi kwa ajili ya maendeleo na Serikali inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria na ili Serikali iweze kukusanya kodi kwa ufanisi mkubwa ni lazima kuwe na Ofisi za TRA katika maeneo mbalimbali nchini:- (a)Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Kilindi? (b)Kwa kutokuwa na Ofisi za TRA Serikali haioni kama inadhoofisha maendeleo ya Wilaya hususani katika suala la mapato? (c)Kwa kuweka Ofisi za TRA Wilaya ya Handeni na kuacha Wilaya ya Kilindi, Serikali haioni kama inawajengea wananchi tabia ya kukwepa kulipa kodi kutokana na umbali uliopo kati ya Wilaya hizo mbili?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni takribani miaka 13 toka Wilaya hii ya Kilindi imeanzishwa. Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana na mimi kwamba, pana umbali mkubwa sana kati ya Wilaya ya Handeni iliko ofisi ya Mamlaka ya Mapato na Kata mbalimbali za Jimbo la Kilindi hususani katika Kata ya Pagwi. Je, ni lini sasa utafiti huu utakamilika ili wananchi wa Kilindi waweze kunufaika na huduma hii? Ahsante.

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa ametaka kujua ni lini utafiti huu utakamilika. Kama nilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba pamoja na utafiti huu kukamilika pia tunaangalia potentials ya ukusanyaji yaani cost and benefit analysis ya kuanzisha ofisi hizi kila Wilaya. Kwa sasa hivi nguvu nyingi tunazielekeza katika kuanzisha ofisi za Mamlaka za Mapato katika mikoa mipya ambayo imeanzishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo naendelea kusema kwamba namwomba Mheshimiwa Kigua aendelee kuongea na wananchi waendelee kulipa kodi kupitia Wilaya yao ya mwanzo kabla ya Kilindi kuanzishwa. Pia tutakapokamilisha utafiti huu na tukaona kwamba kuna potential kubwa ya kupata mapato ya kutosha Wilaya ya Kilindi, basi hatutasita kuanzisha ofisi hii katika Wilaya ya Kilindi na wilaya nyingine zote za Tanzania ambazo hazina Ofisi.