Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Wilaya ya Karagwe ina Sekondari moja tu ya kidato cha Tano na Sita ambayo ni Bugene Sekondari. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Sekondari za Nyabionza na Kituntu ili ziwe shule za kidato cha Tano na Sita?

Supplementary Question 1

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.

(i) Je, Serikali itapeleka lini fedha ilizoahidi kwa ajili ya kujenga mabweni na maktaba pale Bugene Sekondari ambao ni A-level peke yake ya Serikali kwenye wilaya ya watu laki tatu na tisini?

(ii) Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari kuambatana na mimi pamoja na Mbunge wa Jimbo Mheshimiwa Bashungwa ili ukajionee mlundikano wa wanafunzi Bugene Sekondari kwa sababu ya upungufu wa mabweni?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza naomba nianze kujibu swali la pili kwa kwanza nipo tayari tutaambatana pamoja hakika tutaenda kufanya kazi nzuri tu kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifupi niseme nimpongeze sana Mheshimiwa Oliver, kwa sababu yeye na Mbunge Mheshimiwa Innocent wamekuwa wakipambana sana kuhakikisha Halmashauri ya Karagwe inafanya vizuri. Eneo hili ndio maana hata ile shule ya kwanza tuliyoipatia shilingi 190 ni kwa ajili ya maombi yao waliyoyaleta ofisi kuhakikisha tunasaidia wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na upande wa Bugene sekondari tunajua ni wazi kweli idadi ya wanafunzi ni wengi, naomba nikuhakikishie Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunaongeza fedha pale kwa ajili miundombinu ile iweze kuimarika vizuri tuweze kupokea watoto ambao tunatarajia si muda mrefu tutawatangaza. Kwa hiyo, hii ni commitment ya Serikali tutafanya kila liwezekanalo tutaongeza fedha kuimarisha miundombinu ya pale.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Wilaya ya Karagwe ina Sekondari moja tu ya kidato cha Tano na Sita ambayo ni Bugene Sekondari. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Sekondari za Nyabionza na Kituntu ili ziwe shule za kidato cha Tano na Sita?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali, katika jimbo langu la Bunda kuna maboma ya maabara na hasa katika Shule ya Sekondari Salama. Mheshimiwa Waziri hatudhuliani ni ndugu yangu, katika ile shule kumekuwepo na maboma mawili ambayo kuna mabati na mbao zinaenda kuonza ni muda mrefu, wananchi hali yao ni mbaya wamekuwa na michango mingi kwenye maeneo mbalimbali. Nakuomba Waziri hili ni ombi rasmi nakuomba Waziri unisaidie kunipelekea milioni 30 tu kwenye shule ya sekondari salama ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue ombi la Mbunge Boniphace kwa sababu nikifahamu eneo lake lile kwa kweli kuna changamoto nyingi mbalimbali na nikiri wazi kwamba eneo hilo lazima tulipe kipaumbele kwa sababu kuna fedha tu kidogo zinahitajika tutaangalia mfuko ukoje halafu tutashirikiana mimi na wewe kuangalia jinsi gani tutafanya kuhakikisha hiyo miundombinu ambayo wananchi wamejitolea isiweze kuharibika.

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Wilaya ya Karagwe ina Sekondari moja tu ya kidato cha Tano na Sita ambayo ni Bugene Sekondari. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Sekondari za Nyabionza na Kituntu ili ziwe shule za kidato cha Tano na Sita?

Supplementary Question 3

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru shule ya wasichana Nyalanja yenye kidato cha tano na sita ina mchepuo mmoja tu lakini inayo madarasa sita zaidi ya miaka mitano hayatumiki.

Je, Serikali haioni haja ya kutupatia bweni kwa ajili ya kuongeza mchepuo mwingine?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna miundo mbinu kama hiyo, naomba nilichukue jambo hilo kwa sababu hivi sasa ukingalia tuna vijana wengi sana ambao kwa kweli ufaulu umeongezeka. Kwa mfano mwaka huu tuna vijana zaidi laki moja plus ambao wote wanatakiwa wape nafasi kwa ajili ya kidato cha tano na kuendelea. Kwa hiyo, kama kuna fursa kama hiyo ya madarasa yapo tutaangalia nini tufanye ikiwezekana tukatafute fedha kwa haraka tuongeze pale bweni kwa ajili kuhakikisha kwamba tunaongeza mchepuo mwingine vijana wengi wa kitanzania waweze kupata nafasi.

Name

Maryam Salum Msabaha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Wilaya ya Karagwe ina Sekondari moja tu ya kidato cha Tano na Sita ambayo ni Bugene Sekondari. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Sekondari za Nyabionza na Kituntu ili ziwe shule za kidato cha Tano na Sita?

Supplementary Question 4

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakipata mimba katika mazingira magumu.

Je, Serikali ina mikakati gani kujenga hostel za watoto wa kike ili wapate kujistiri waondokane na vishawishi vya barabarani?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ndio maana azma ya Serikali juzi juzi mwezi wa tatu Serikali imetoa takribani shilingi bilioni 54.6 ambayo katika hili lengo lake ni kujenga madarasa takribani 988 lakini mabweni mapya 210 kwa hiyo ni commitment ya Serikali kuhakikisha jinsi gani mabweni haya yanjengwa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa dada yangu naomba nikuhakikishie kwamba tutafanya kila liwezekano tutaangalia nini tufanye licha tunaanza kujenga mabweni 210 katika maeneo mbalimbali lakini juhudi ya Serikali itaendelea kuhakikisha vijana hawa wa kike tunawaondoa katika hali hatalishi zaidi hasa kwa watu ambao wana nia mbaya kuhakikisha wanaharibu future ya watoto wa kike. Kwa hiyo, tunaendelea kulichukua kwa ajili ya Serikali kulifanyia kazi.