Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO Aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya viongozi kutoka nje ya nchi wanaokuja Tanzania na kutembelea baadhi ya maeneo na kisha wanapokuta miradi ya wananchi huahidi kusaidia na baadae kushindwa kutimiza ahadi zao?

Supplementary Question 1

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza kabisa pia nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wetu kuweza kuirudisha ndege yetu Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la nyongeza litakuwa moja; je, Waziri anaweza kutuambia ni njia gani zinazotumika kwa viongozi wa Wilaya na Mikoa kufuatilia ahadi zinazotolewa na viongozi hawa wanapokuja nchini? Ahsante.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Tauhida kwa kazi nzuri ambayo anaifanya kule Zanzibar akiwakilisha wananchi. Amefanya mambo mengi, ametoa kompyuta na kujenga madarasa ya kompyuta na amekuwa akijulikana kama ni rafiki wa wanawake na watoto. Swali lake ni ushahidi tosha kwamba anafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar inashirikiana kwa karibu kabisa na viongozi wa Wilaya na Mkoa pamoja na Ofisi ya Rais kule Zanzibar, katika kufanya vikao vya mashauriano ili kuona kwamba ahadi ambazo zimetolewa na hazijatekelezwa zinatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, niwashauri Mheshimiwa Tauhida tuendelee kushirikiana kupitia viongozi wa Wilaya, Mkoa, Wizara za Kisekta, Ofisi ya Rais Zanzibar pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha kwamba ahadi zote zinatekelezwa. Kama kuna ahadi sugu ambayo haijatekelezwa nitamuomba tuonane ili tuweze kuitekeleza haraka iwezekanavyo.