Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Kijiji cha Sojo katika Kata ya Isugule, Wilayani Nzega patajengwa Kituo kikubwa (coating yard) cha kuandaa mabomba yote ya mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga ambapo Kituo hicho kitakuwa na wafanyakazi zaidi ya 2,000; kutokana na ongezeko hilo la idadi ya watu mahitaji ya huduma za Jamii yatakuwa makubwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Kituo kidogo cha Polisi katika Kijiji cha Sojo ili kuhakikisha usalama kwa wananchi na mali zao?

Supplementary Question 1

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Kwa kushirikiana na Mwekezaji anayejenga hii Coating Yard pale Sojo Igusule, Kijiji cha Sojo Igusule tumefaidika kwamba sasa tutapata maji kwa msaada wa huyu mwekezaji na pia tutapata umeme kwa haraka kuliko ulivyokuwa kwenye mpango, lakini pia kituo cha afya cha pale, kitakuwa upgraded kuwa kituo cha afya cha kisasa. Sasa swali langu ni kwamba, je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kufanya mazungumzo na huyu mwekezaji anayejenga hiyo coating yard pale, kwa sababu atawekeza zaidi ya bilioni 600 na hivyo na yeye pia atahitaji masuala ya usalama? Je, Serikali iko tayari kufanya naye mazungumzo ili na yeye achangie ujenzi wa hicho kituo cha polisi kama ambavyo amechangia kuleta maji, umeme na kupandisha hadhi kituo cha afya?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Selemani Zedi, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya jimbo lake kwa ajili ya kuweza kueneza huduma mbalimbali za kijami katika jimbo lake. Kuhusiana na wazo ambalo amelitoa, pia ni wazo zuri, lakini nataka nimjulishe kwamba, wazo hilo siyo geni, kwa mfano katika Mradi wa Stiegler’s Gorge ambao unaendelea kule Rufiji, tumefanikiwa kupata kituo, tupo katika mchakato wa ujenzi wa kituo cha polisi, ambapo unatokana na mradi huo. Kwa hiyo, tutatumia mawazo yake pamoja na mbinu ambazo tumetumia kule Stiegler’s Gorge kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wawekezaji hao waliopo katika jimbo lake wa mradi huo wa bomba la gesi ili tuone uwezekano wa wao kushiriki kusaidia ujenzi huo wa kituo cha polisi.