Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joyce Bitta Sokombi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOYCE B. SOKOMBI (K.n.y. MHE. ESTHER N. MATIKO) aliuliza:- Serikali imekuwa ikitoa vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya Tsh. 4,000,000/= kila baada ya miezi mitatu kwenye zahanati za Halmashauri za Mji wa Tarime kupitia Wakala wa dawa (MSD); kwa miaka miwili iliyopita Serikali imepunguza ugawaji wa dawa na vifaa tiba kutoka thamani ya Tsh. 4,000,000/= mpaka Tsh. 166,000/=; mfano zahanati ya Gamasara imepokea dawa na vifaa tiba vyenye thamani hiyo:- Je, ni kwa nini Serikali iliamua kupunguza mgao wa dawa kutoka Tsh. 4,000,000/= mpaka Tsh. 166,000/= ilhali idadi ya watu inazidi kuongezeka katika Halmashauri ya Mji wa Tarime na Majimbo ya jirani?

Supplementary Question 1

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda tu kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Zahati ya Kenyamanyori ambayo inatoa huduma kwa Kata mbili ambayo ni Nyandoto na Ketare. Wananchi wa maeneo yale wamejitolea kwa nguvu zao, wamejenga jengo la wazazi ambalo ni kiliniki ya wanawake kufikia lenta, pia nguvu ya Mbunge, ameweka pake mifuko 20: Je, ni lini Serikali, itaongeza nguvu kuweza kufikia kumaliza jengo lile la kiliniki ya mama na mtoto? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili: Je, ni lini Serikali itapeleka dawa katika Zahanati ya Gamasara kulingana na kiasi cha fedha kilichobaki MSD?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Zahanati ya Kenyamanyoli kuna nguvu ya ujenzi inaendelea pale na kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema, lakini kwa mwaka huu wa fedha Halmashauri ya Mji wa Tarime imetenga fedha lakini kutoka kwenye Bajeti ya Serikali Kuu tutaangalia kitachowezekana ili kusaidia nguvu za wananchi hawa ambao wamejitolea ili nguvu yao isiweze kupotea bure. Kwa hiyo, tuendelee kuwasiliana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI tuone tunafanya kitu ili kuongeza nguvu watu wote katika eneo hili waweze kupata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anauliza kama tunapeleka dawa kwa fedha ambayo imebaki. Nimesema katika jibu la msingi kwamba waliomba milioni 17, bado zimebaki milioni 13. Wizara hatuna shida kupeleka madawa katika Zahanati hii wala mahali pengine popote pale, maelekezo ya Serikali ni kwamba kadri ambavyo bajeti imepangwa mahitaji ya wananchi ni Watumishi wetu katika eneo hili wajitahidi kuagiza dawa, dawa zipo kwa hiyo kama wanauhitaji fedha zimebaki zipo ni wao wapeleke madai yao tutoe maelekezo, wananchi wa Kamasala, Kenyamanyoli na maeneo mengine waweze kupata huduma ambayo ilitarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)