Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hasna Sudi Katunda Mwilima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. HASNA S. K. MWILIMA aliuliza:- Tarafa ya Nguruka ina wakazi zaidi ya 100,000 na ndio kitovu cha biashara:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka umeme wa Grid ya Taifa kutoka Usinge, Wilaya ya Kaliua? (b) Wakazi wa Kata za Mwambao, Sunuka, Kaliya, Buhigu, Igalula, Haramba na Sigunga hawana umeme na Jiografia ya kuwaunganishia umeme kutoka Uvinza ni ngumu. Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka umeme kutoka Mpanda, Mwese kwenda Kata ya Kaliye, ili iwe rahisi kuzipitia kata zingine?

Supplementary Question 1

MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake, natambua kazi nzuri wanayoifanya. Ni kweli kabisa kwamba, Nguruka pale tulitoa ekari 30 kwa ajili ya ujenzi wa hiyo substation, lakini Meneja wa TANESCO alienda, hadi leo utekelezaji haujaonekana. Sambamba na hilo mwaka jana mwezi wa Nane mkandarasi alifanya survey katika Kata ya Nguruka, Kata ya Mtego wa Noti, Kata ya Itebula, Kata ya Mganza, Kata ya Sunuka, sambamba na vijiji ambavyo vilisahaulika kwenye Mradi wa REA awamu ya pili. Swali langu. Je, Wizara hii mnawaambia nini wananchi wa kata hizi, ni lini mkandarasi atapeleka materials ili sasa utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu uweze kuanza rasmi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, natambua kwamba, kuna mazungumzo baina ya mwekezaji kutoka Marekani pamoja na Wizara ya Nishati kufua umeme kwenye Mto Ruwegere uliopo kwenye Kijiji cha Mgambazi, Kata ya Igalula. Sasa wananchi wa Kata ya Buhingu, Kata ya Herembe, Kata ya Sigunga na Kata ya Igalula yenyewe wanataka kusikia Kauli ya Serikali. Ni lini sasa mkandarasi huyu ataanza rasmi kutekeleza uzalishaji wa kufua umeme kwenye Mto Ruwegere, megawati tano? Nataka majibu ya Serikali.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ufafanuzi wa swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge kwa vile ambavyo amelieleza. Napenda pia nimpongeze Mheshimiwa Mbunge jinsi ambavyo anafuatilia masuala ya nishati kwa wananchi wa Uvinza. Baada ya kusema hayo napenda sasa nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hasna Mwilima, Mbunge wa Maeneo ya Uvinza, Jimbo la Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kabisa mkandarasi alipata kazi dakika za mwisho ukilinganisha na mikoa mingine. Hata hivyo, napenda nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge na jinsi anavyofuatilia, hivi sasa mkandarasi ameshaanza ku-order materials na ataanza kupeleka materials kwenye eneo la Uvinza kuanzia tarehe 22 mwezi huu. Maeneo yatakayopelekewa ni pamoja na Kazuramimba, Ilagala, Kajeje kuelekea Sunuka, lakini pia maeneo ya Nguruka na katika maeneo mengine ya Uvinza ambayo hayajapelekewa nishati ya umeme. Maeneo yote 27 ya kwa Mheshimiwa Mbunge yatapelekewa umeme ndani ya miezi tisa ijayo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nimpe tu uhakika kwa wananchi wa Uvinza kwamba, mkandarasi amesha-mobilise material na kuanzia tarehe 22 mwezi huu ujenzi utaanza rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la pili, ni kweli kulikuwa na mkandarasi aliyetarajia kufanya survey kwa ajili ya kuzalisha umeme megawati nane katika Mto Rwegere, lakini taarifa za awali baada ya kupewa kazi na baada ya kufanya tathmini za awali inaonesha Mto Rwegere unaweza kutupatia megawati tano kutokana na maporomoko ya maji ya Mto Rwegere.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kazi inayofanyika mara baada ya kuleta taarifa mkandarasi amefanya mapitio na wataalam wetu, ni matumaini yetu kwamba, mwezi ujao atatuletea taarifa za mwisho, ili kuona kama mradi huo utakuwa na tija na kuzalisha megawati tano. Kwa hiyo, nimpe pongezi Mheshimiwa Mbunge kwamba, hiyo kazi inatushirikisha sana, inaendelea vizuri na tunaweza tukapata megawati tano mbali na megawati 45 za Mto Malagarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani kidogo niongeze kwenye mradi muhimu sana kwa Kigoma, ujenzi wa transmission line kutoka Tabora kupita Urambo kwenda mpaka Nguruka hadi Kidahwe umeshaanza. Tunatarajia mkandarasi atakamilisha kazi Februari mwakani ili wananchi wa Kigoma waweze kupata umeme wa gridi nao kutoka umeme wa gridi unaotoka Tabora wa kilovoti 120. Nimeona nilifafanue kwa sababu, sasa hivi clearance ya major substation inafanyika Urambo na wiki inayokuja itafanyika Nguruka na Kidahwe wanamalizia mwezi ujao. Hiyo ni taarifa kwa ajili ya umeme wa wananchi wa Kigoma. Ahsante sana.